26 Machi 2015 - 18:18
Ufaransa yashambulia magaidi wa Daesh Tikrit

Ufaransa imeshambulia maeneo ya wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh katika eneo la Tikrit nchini Iraq kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mashambulio ya kimataifa dhidi ya wanamgambo hao wa kundi la kigaidi.

Ufaransa  imeshambulia  maeneo  ya  wapiganaji  wa  kundi la kigaidi la Daesh katika  eneo  la  Tikrit  nchini  Iraq kwa  mara  ya  kwanza tangu  kuanza  kwa  mashambulio  ya  kimataifa  dhidi  ya wanamgambo  hao  wa  kundi la kigaidi. 

Msemaji  wa  serikali  ya  Ufaransa  hakutoa  maelezo  zaidi  ya iwapo  ndege  za  kijeshi  ama  ndege  zisizokuwa  na  rubani zilitumika  kufanya  mashambulio  hayo, na  amekataa  kutoa maelezo  zaidi  kuhusu  maeneo yaliyoshambuliwa.

Majeshi  ya  Marekani  yametangaza  hapo  kabla  kufanya mashambulizi  ya  anga  dhidi  ya  maeneo  ya  kundi la kigaidi la Daesh mjini  Tikrit pamoja  na  majeshi  ya  muungano  baada ya kumuomba  waziri mkuu  wa Iraq  Haider al-Abadi awaruhusu kufanya mashambulizi hayo.

Maelfu  ya  wanajeshi  wa  Iraq , maafisa  wa  polisi  na  jeshi  la anga   wamewekwa  ili  kuukamata  mji  wa  Tikrit , ambao wapiganaji  wa  kundi la kigaidi la Daesh wanajitahidi  kuulinda  kwa  kutega  mabomu mitaani  pamoja  na  majengo  mbali  mbali  ndani  ya  mji  huo.

Ushindi wa majeshi ya Iraq katika mapambano hayo unatokana na msaada wa pekee kutoka kwa Jeshi la Quds la Iran likiongozwa na Meja Jeneral Qassim Suleiman.